Asubuhi moja hivi nilipoamka nikakutana na simu kutoka kwa
rafiki yangu, dada yangu na moja kati ya watu ambao nawa-admire sana. Akili yake,
Moyo wake, Uhuru wake na ufanya kazi wake ni vitu amabavyo vinamfanya awe wa
manufaa sana kwangu, na kwa taifa na hata ulimwengu kwa ujumla wake.
Ilikua ni mada flani nyeti sana na binafsi iliniongeza kilo
za ufahamu na uimara wangu kwa ujumla. Alikua ananitazamisha juu ya PURPOSE,
MAHUSIANO/NDOA, MTU KUWA COMPLETE na namna haya mambo yalivyoumbwa kwenda
pamoja.
Unajua PURPOSE ndio ulimwengu wako. Tunakufahamu na kukupata
unapokua katika PURPOSE ya maisha yako! Kila mtu ana kitu anataka kukitimiza.
Ndoto, wazo, lengo! Na ni safari mpaka kufika katika utimilifu wake! Safari
Fulani ambayo njiani kuna mambo mengi sana. Lakini mambo hayo yote kwa ujumla
wake, yanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba unafika unapotaka kufika katika
uimara unaohitajika.
Sasa changamoto inakuja pale mtu hajui anaelekea wapi, au
hajatambua yeye anaisha kutimiza ndoto gani ama kujenga jambo gani! Halafu
anajikuta kwenye mahusiano bahati mbaya zaidi na mtu ambaye anafanana na yeye
(wote mpo kwenye upofu na giza zito la “PURPOSE of your lives/What you are
living for!”
Mahusiano Bora yanatengenezwa na vitu viwili au zaidi vilivyo
WELL ESTABLISHED, GRAUNDED, FOCUSED TOWARDS A CERTAIN GOAL. Mahusiano
hayajengwi na pande mbili zilizo nusu nusu na zinazohitaji upande mwingine
kujikamilisha. Ukiwa hujakamilika tayari ni tatizo kwenye mahusiano! Hata Gari,
LINA ENGINE ILIYO KAMILI, TAA ZILIZO KAMILI, MATAIRI, N.K Na hivi vitu katika
ukamilifu wake ndivyo HUFANYA GARI KAMILI LENYE UIMARA NA UMARIDADI WAKE.
Hizi Methali za Mwanaume hajakamilika bila mwanamke
zinatupeleka chaka. Huyu Mwanadada alinipa mfano mmoja ambao upo katika vitabu
vya kiimani, juu ya Adam na Hawa. Mwenyezi Mungu Hakumuumba hawa kwa sababu
Adam akikua hajakamilika! MWENYEZI MUNGU ALIMPATA HAWA KATIKA ADAM (EVE WAS IN
ADAM ALL ALONG, ADAM WAS COMPLETE). Hakumuumba Hawa kwa sasbabu Adam alishindwa
Majukumu! Adam aliyamudu vyema majukumu yake ndipo Mungu akawaza Kumfanyia
Msaidizi. (Kama hujayajua majukumu yako utajuaje ni msaidizi yupi anayekufaa)
(Kama hujayamudu majukumu yako utafanyiwa vipi msaidizi)
Sio Adam aliyetaka Msaidizi, Ila Mungu ndiye aliyemuwazia
kuhusu msaidizi. Sasa wewe utakosea sana pale unapokua unataka Msaidizi bila ya
kuwa na cha kusaidiwa. Una-qualify kupata Msaidizi pale unapokua huhitaji
msaidizi, na ukiona una mshawasha wa msaidizi ujue huja-qualify kupatiwa
msaidizi.
Loneliness (Upweke) ni moja kati ya gia inayowasukuma wengi
sana Kwenda kwenye mahusiano na hata ndoa! Ila ukweli ni kwamba Upweke ni
ugonjwa! Kama huwezi kujifurahia mwenyewe basi uwe na uhakika hata mtu mwingine
hawezi kukufurahia. Upweke ni kirusi Fulani hivi ambacho ukiingia nacho kwenye
mahusiano hakitayaacha mahusiano katika hali salama.
Huwezi kuwa na mtu kabla hujaweza kuwa na wewe mwenyewe! Na
unakua na mtu pale unapokua na wewe mwenyewe! Na njia pekee salama ni KUANZA
KUWA NA WEWE MWENYEWE KABLA YA MTU KUWA NA WEWE.
Kutaka mtu kwenye maisha yako ni ishara ya kuwa umejichoka.
Na kama wewe mwenyewe umejichoka, nani ambaye hatakuchoka? Nakumbuka moja ya “Quotes” zangu, iliyotokea
kupendwa na wengi inasema “Lonelyness is not a sign that you need someone, it’s
a sign that you need yourself” (Upweke si ishara kwamba unahitaji mwenza, ila
ni ishara kwamba unajihitaji mwenyewe)
Unapata mwenza kwa kujipata wewe mwenyewe. Kama hujajipata
utakua unajaribu kila kitu na utatafuta kila mahali! Utafikiri kuwa
hawapatikani au hawapo ila UKWELI NI KWAMBA WEWE NDIO HUJAPATIKANA. (Hujasikia
lugha za: Wanawake wa siku hizi hakuna kitu kabisa… Wanaume wa siku hizi ni
mashetani kabisa) (Imagine huyu mtu anayeishi kwenye huu ulimwengu wa “Wanawake
hakuna kitu” “wanaume ni mashetani”, AMECHOKA NA ANACHOSHA SANA)
Mwenza bora ni Yule unayekutana naye kwenye Purpose ya maisha
yako. Ukweli ni kwamba watu hawabadiliki (Ile unasikia Mwanaume/Mwanamke wangu
kabadilika) ila ni vile unakuwa umempata mtu kabla hajajipata yeye mwenyewe
(KUPATWA KWA MTU HAHAHA)
WASHKAJI, MAKE YOURSELF COMPLETE! It is when you don’t need
someone to complete you; your eyes will be open to SEE WHO YOU NEED.
Mahusiano sio msimu wa LIGI kwamba lazima na wewe ushiriki.
Umri, Fedha, Eneo, marafiki, haviamui mahusiano yako! Ila Purpose yako ndio
YAPASWA KUAMUA mahusiano yako. HUCHAGUI WA KUHUSIANA NAYE ILA WA KUHUSIANA NAYE
HUCHAGUKLIWA NA “PURPOSE” YA MAISHA YAKO.
Cheers!
0 comments:
Post a Comment