MAZOEZI YA MWILI NA FAIDA ZAKE (KWA MUJIBU WA SAYANSI) KATIKA AKILI, HISIA NA FIZIKI

Tungeweza kuita uchawi wa sayansi ya matibabu, ila kwa kuwa sayansi haina uchawi basi tuiite dawa yenye uwezo usioelezeka. Ni kitu ambacho tumekisikia mara kwa mara na wote tumekubaliana nacho kwa ukweli kwamba ni cha umuhimu! Ila wachache huzingatia. MAZOEZI NA KAZI ZINAZOSHUGHULISHA MWILI vina uhusiano wa karibu sana na Hali ya afya ya mwili.
Imethibitika kisayansi kuwa Hakuna matibabu yenye kutoa matokeo makubwa kwa mwili, akili na hisia kama mazoezi ya mwili (ikijumuisha michezo pamoja na kazi zinazohusisha viungo vya mwili kufanya kazi)
Leo katika Makala hii kwenye kipengele cha Afya (kenye labels za blog yetu unaclick Health) Tunakuletea faida ambazo pengine wengi wetu tulikua hatuzifahamu kuhusiana na Jinsi mazoezi ya mwili huleta matokeo ya kimatibabu katika mwili wa mwanadamu.
Faida hizo ni zifuatazo:
  1. Mazoezi huongeza uwezo wa kuishi muda mrefu na kuimarisha uwezo wa kujikinga na magonjwa kama Shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, Stroke, Kisukari aina ya pili (Type 2 Diabetes), Kansa ya Matiti, na mengine mengi.

  1. Huongeza Ufanyaji kazi na uhusiano kati ya Moyo, Mapafu (Cardiorespiratory) na uimara wa misuli: Hii husaidia sana katika kazi mbalimbali za kila siku na stamina ya mtu katika kazi.

  1. Huwezesha mmeng’enyo wa chakula kwenda inavyopaswa na pia husaidia sana kupunguza uzito wa mwili. Mazoezi ya mwili hufanya wmili wako kuhitaji chakula Zaidi lakini katika kula kiasi kikubwa cha chakula mwili hauwi mzito. (you eat more and maintain a constant weight)

  1. Pia Mazoezi ya mwili husaidia kupunguza Msongo wa mawazo (Stress), Hofu, na unyogovu (depression), na Hukupa Mood nzuri
  1. Husaidia ubongo kufanya kazi vizuri Zaidi, haswa kwa watu wazima.  Tafiti zinasema kwa kadri mtu anavyozeeka, Ubongo hupungua uwezo wa kufanya kazi. Hivyo haswa kwa watu wa kuanzia miaka 45 na kuendelea mazoezi ya mwili au kazi za kuhusisha viungo vya mwili huleta matokea makubwa katika uwezo wa ubongo kufanya kazi. Sio kwamba kwa watoto na vijana mazoezi ya mwili hayasaidii ubongo kufanya kazi kwa ubora Zaidi, La! Yanasaidia; ila ni vile kwa watu wenye umri mkubwa ubongo wao unakua umeanza kupoteza uwezo wa kufanya kazi kama ulivyo ubongp wa kijana au mtoto.

  1. Pia mazoezi ya mwili huimarisha mifupa na sehemu za maungo ya mwili wa mwanadamu. Hii husaidia sana na hata matabibu hushauri sana watu wenye matatizo ya magoti na maungio ya mwili, kujihusisha na mazoezi ya mara kwa mara.

  1. Usingizi mnono ni mojawapo ya faida za kuufanyisha mwili kazi au/na mazoezi. Watoto hulala vizuri mwili unapokua umechoshwa na mazoezi, vijana vilele na hata watu wazima. Kama huwa unapata changamoto ya kupata usingizi, basi mazoezi ya mwili yanaweza kukusaidia sana kukabiliana na changamoto hii.

  1. Lakini pia wanasaikolojia wamebaini kuwa Mazoezi ya mwili huongeza ujumla wa ubora wa kiwango cha maisha (overall quality of life). Hata huku mitaani kwetu, ukimuona mtu anafanya mazoezi basi kwanza lazima umuhisi kuwa ana uwezo kiuchumi na pia ni msomi, kumbe inaweza hata isiwe hivyo! Ki ujumla humsaidia sana mwanamazoezi kuridhika na hali ya maisha na hata kuinua kiwango chake cha maisha. Wanamazoezi wengi wana nafasi kubwa ya kuinua kiwango cha furaha, mafanikio na kuridhika kimaisha kuliko wasio na kawaida ya mazoezi.

  1. Mazoezi pia huongeza au hurudisha hali ya hamu ya tendo la ndoa. Ni changamoto kwa baadhi ya ndoa haswa linapokuja swala la tendo la ndoa; hamu ya kulitenda; kufurahia tendo la ndoa; na kuridhika na tendo la ndoa. Mazoezi ya mwili yamethibitika kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto hii. Kwa mujibu wa tafiti moja ya chuo cha udaktari huko Austria, imethibitika kuwa wanandoa wenye kawaida ya kujihusisha na mazoezi huwa na furaha Zaidi na hamu ya tendo la ndoa ikilinganishwa na wale wasio na kawaida ya mazoezi ya mwili. Mtu anapokua katika hisia za kufanya tendo la ndoa, msukumo wa damu huongezeka kuelekea kwenye nyeti zake. Vile mzunguko au msukumo wa damu unavyokwenda sawia ndivyo hivyo hivyo hata tendo linakwenda sawia (when a person is aroused, blood flows and rushes into genitals. Hence the better the circulation, the less likely one is to suffer from sexual dysfunction). Vile vile kwa wanaume ambao hufanya mazoezi mara kwa mara, hawako kwenye uwezekano wa kupata shida ya mshindo kama INAVYOWEZA ikatokea kwa wanaume wasiofanya mazoezi. NB: ifahamike kwamba hili si tatizo au ugonjwa, ila ni vile mazoezi ya mwili huweza kukusaidia kuboresha uwezo wako wa kukabiliana na tendo la ndoa. Mwisho katika pointi hii ni uhalisia kwamba, mwili wa mazoezi huvutia Zaidi kuliko ule usio wa mazoezi.

  1. Tuje kwenye faida namba kumi kwamba mazoezi ya mwili hufanya siku yako kuwa maridhawa na siku inayofuata kuwa na ubora katika utendaji wa shuguli za siku.
  1. Pia mazoezi ya mwili hufanya ngozi kuwa na afya. Oksijeni na virutubisho vingine husafirishwa kwenda kwenye seli za damu (tunafahamu vile mazoezi ya mwili huongeza msukumo na mzungukowa damu) na vile vile huruhusu taka mwili kutolewa nje. Hivyo kuiacha ngozi yako ikiwa na afya.
Kwa leo tuishie hapa, hadi wakati mwingine. Endelea kufatilia Makala zetu zitakazokuwa zinahusiana na afya na Makala nyinginezo za kuelimisha, kuhamasisha na kutazamisha; ili kutufanya watu bora katika ubora usiopungua; Ni kupitia blog yetu hii lighttz.blogspot.com. Lakini pia ukurasa wetu wa facebook: facebook.com/thelighttz. Instagram:thelighttz na twitter: teamlighttz. Asante, Hongera kwa kujifunza na karibu tena.

Share on Google Plus

About The Light