MAMBO FULANI MUHIMU SANA KUYAFAHAMU HASWA UNAPOKUA KIJANA WA MID 20's - Frazier Light




Unapofikisha miaka 22-25 au NA KUENDELEA, mambo mengi sana huanza kubadilika. Mtu huanza kujua nini anataka kwenye maisha na pengine baadhi wanakua ndio wameanza kuajiriwa na kujiajiri. Ni kipindi Fulani ambacho japo bado unakuwa kijana, akili na saikolojia yako huanza kufikiri tofauti. Nguvu ya kuanza kufanya mambo ambayo ulikua hudhani kama unaweza kufanya, huja! Na aibu huanza kuondoka. Woga huweza kuwa mwingi na stress za mara kwa mara, haswa pale unapokutana na changamoto na usijue kama kesho yako yaweza kuwa bora! Yote tisa ila kumi, ni umri muhimu sana kwa maisha ya kila mtu. Tunaweza kusema ni “turning point” ya maisha ya mtu, hivyo ni vyema ukatambua namna ya kujiendesha haswa unapokua katika umri huu. Ni umri poa sana kwa hiyo jiweke sawa kuufurahia katika namna yake.
Sambamba na haya kuna mambo mengine mengi ambayo huna budi kuyaweka sawa ili kuwa na “FUTURE” unayoitaka kutoka moyoni. Yafuatayo ni mambo kadhaa ambayo naamini ni ya umuhimu sana tukayafahamu.
  1. Anza kuzingatia muonekano wako haswa katika mavazi. Kila shughuli ina namna yake ya kutokea, mazingira nayo yana namna yake ya kukutaka uonekane. Ni vyema ukaanza kuzingatia muonekano wako kulingana na shughuli au tukio Fulani unalo/utakalohudhuria. Ina mchango mkubwa sana kwenye vile utakavyokua unajichukulia wa umuhimu, wa kujiheshimu na itakua hivyo! Watu watakuheshimu na kukuona wa umuhimu Pia. Pa suti vaa suti, pa kuchomekea chomekea, pa gauni vaa gauni, pa pedo vaa pedo, pa pensi vaa pensi, vyovyote vile ili mradi uendane na shughuli husika na uwe “comfortable” kwa sababu ni muhimu kuwa “comfortable” na mavazi yako.

  1. Achana mahusiano ambayo unajua kabisa hayana future. Ni ngumu kumpata mtu ambaye anaweza kujenga future pamoja na wewe. Ila hata kama bado hujampata, atleast kuwa na idea ya mtu wa namna gani unamuhitaji kwa future yako. Anza kuji-train namna ya kutulia kama ulikua hujazoea kutulia. Anza kujifunza na kusoma mambo ambayo yatakusaidia kujenga mahusiano yenye furaha na mafanikio.

  1. Jifunze kutokujali sana watu wengine wanakuonaje. Huu ni umri ambao kila mtu atakuwa na matarajio yake kwako, ila lazima uelewe kwamba vile unavyojiona, kujipangilia na kujijua ndio kitu cha muhimu. Ni kawaida sana kwa mwanadamu yoyote kusumbuka na vile watu wanamuona au wanafikiri kuhusu yeye! Watu wengi sana wanakosa usingizi na hata wengine wana give-up kwenye njozi za maisha yao na mipango yao, ili tu waishi kuendana na matarajio ya wengi. USIWE MMOJA WA HAWA WATU! Haitakupa matokeo unayoyataka kwa maisha yako.

  1. Acha kuwalaumu wazazi wako. Naomba ufahamu hili, hakuna mzazi wa mtu ambaye hakukosea sehemu, hata wewe ukiwa mzazi siku moja utaona vile ambavyo utakua unakosea mara kwa mara. (ushauri wa bure, confront makosa na omba radhi hata kama ni kwa mtoto wako). Kulaumu wazazi wako kwa kosa ambalo wewe unajua walifanya au wanafanya aidha wanatambua kwamba wanakosea au hawatambui, haikusaidii chochote Zaidi ya kuvunja uhusiano na familia yako. Kama wamekosea, FIX it! Na ujifunze ili usije ukafanya kosa kama hilo kwa watoto wako.
  2. Acha kujilaumu kwa njozi ambazo hukuweza kuzitimiza. Ukiuliza watu wengi leo, watakwambia nilivyokua mdogo nilitaka kuwa Daktari, ila (atatoa kisingizio au sababu iliyomkwamisha)…. Nikwambie tu, hata mimi nilitaka kuwa daktari; Ila leo mimi si daktari, na wala sitamani ningekuwa daktari, ila natamani ningekuwa hivi hivi nilivyo leo. Kila mtu ana njia yake kwenye maisha, na hakuna hata mmoja, hata mmoja atakayekuwa na maisha yanayofanana na mwingine. Hata kama mtakuwa na kipato sawa. Kila mtu ana bustani yake ya edeni, ana eva/adam wake na ana nyoka wake (na mimi nakumbuka kumbuka biblia kidogo). Ni jukumu lako kupanda future unayoitaka, kuipalilia na kuitunza na kuhakikisha hujioni uchi)

  1. Kuwa mkweli kuhusu hali yako kiuchumi. Miaka hii ni kipindi ambacho mambo hayatakuwa kama vile ambavyo ulidhani yatakuwa. Kama unaanza kujenga uchumi wako na kujitegemea ni kawaida sana kuishiwa kabisa, ni kawaida kulala njaa, inatokea/itatokea, ni kawaida kusaidiwa au kupiga vizinga, ni kawaida. Ila sio ishu, kikubwa jua unajenga nini na weka nguvu na bidii yako yote! HAKUNA LISILOWEZEKANA. Usidanganye kwamba una hela kumbe huna, haitakusaidia. Ila be honest with yourself na huna sababu ya kumficha mtu hali yako kiuchumi kama atataka kujua kwa sababu za msingi. Kuwa free kutokutoa michangio ya harusi pia! Lol. Na hii point ni muhimu sana haswa kwa wale wenye mahusiano, usimfiche mpenzi wako kwamba HUNA HELA NA PIA UJUE ANA HAKI YA KUHOJI KWA NINI HUNA HELA, so jipange kwa majibu yenye tija. VILE VILE, kama mkondo wa pesa umeanza kukugeukia, jifunze kuweka akiba na hata kuwekeza. Katika umri huu ni muhimu sana kufanya hivi.

  1. Jifunze kusema HAPANA. Ukiwa na umri wa miaka kumi na mpaka ishirini hivi, unakua mwepesi kuvutwa na kila kitu na pia kumsikiliza kila mtu. Ni jambo zuri, na kwa kiasi linakujenga. Ila ukifikisha umri huu wa mada yetu ni vyema kuwa mtu wa maamuzi siyo wa kuamuliwa! Ni vizuri kushauriwa na kusikiliza ushauri lakini hakikisha unauchambua na kufanya maamuzi yako binafsi. Wewe ndio unayejua vizuri nini unaweza kwa kiwango gani na nini huwezi. Kusema hapana siyo kiburi ila ni kujiheshimu.

  1. Acha kuanika maisha yako mtandaoni. Ni Ushamba, ni utoto na muda wake umeshapita. Ni muhimu ku-share na marafiki zako fikra zako, ni muhimu kushare nao picha na matukio mbalimbali, ila kuna mambo ya siri (kama wewe kugombana na mpenzi wako) au (wewe kuwa na uadui au chuki na mtu Fulani) jifunze kuheshimu mikusanyiko ya wengi kama mitandao ya kijamii. Vile vile ni umri ambao kama huna kazi zinazohusisha mtandao, ni vyema kupangilia muda wako unaoutumia mtandaoni. Hii ni ngumu sana kwa wengi ila ni muhimu sana kama unataka kuwa mtu ambaye wakati wote unapiga hatua hata kama ni hatua kidogo.

  1. Acha kutokujijali! Unapofika umri huu utaanza kukumbuka vile ambavyo ukiwa na miaka 18-22 hivi ulikua unaweza kukesha night club na kulala kesho yake siku nzima, kwani mwili unakua umechoka sana. Au ulikua unaweza kutumia kilevi bila kipimo, au kuvuta bila kipimo. Unapofika umri huu ni vizuri ukawa unajali afya yako. Lala muda wa kutosha, punguza au acha kabisa kunywa vinywaji vyenye au kuvuta kemikali na vitu vinavyodhuru mwili na akili. Badala yake ni muhimu kuamka mapema na kufanya vitu vinachoihitaji akili yako kwani asubuhi akili huwa vizuri Zaidi.  Fanya mazoezi pia. Hii ni nzuri sana kwa akili, hisia na mwili wako. Unaweza pia ukasoma Makala yetu yenye kichwa kinachosema “Body Exercizes and physical, emotional and mental health” mtaalamu wetu ameeleza kwa undani sana faida zilizothibitishwa kisayansi na kisaikolojia, zitokanazo na kuufanyisha mwili mazoezi. Makala hii imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili isipokua kichwa cha habari.

  1. Tuhitimishe kwa kusema kwamba, ni vyema pia ukaanza kuwa mtu wa kujipangilia na kupangilia mambo yako. Mpangilio unaanza katika mambo madogo madogo tu, mswaki ukae mahali pake, viatu vikae mahali pake, Nguo zikae mahali pake, weka mambo yako na ratiba zako katika namna ya kueleweka ili usiwe unatumia masaa kutafuta kitu chako ambacho hukumbuki mara ya mwisho ulikiweka wapi.

Usisahau pia, unaweza ukawa wa kwanza kupokea Makala zetu kwa ku-”subscribe” kwa email yako. Makala zetu zipo katika lugha ya Kiingereza na nyingine kama hii kwa lugha ya Kiswahili, siyo tabu kwani katika blog yetu (lighttz.blogspot.com), unaweza kusoma Makala zetu kwa lugha Zaidi ya 50 kwa kubofya “Translate” upande wa kulia chini ya kiboksi cha facebook. Vile vile ili kupata updates za msingi, na quotes zitakazokujenga kumbuka ku-like ukurasa wetu wa facebook: facebook.com/thelighttz, twitter: teamlighttz na Instagram: thelighttz na unaweza pia kutuandikia kwa email: the.light.tz@gmail.com . ASANTE NA HONGERA KWA KUJIFUNZA



Share on Google Plus

About The Light

0 comments:

Post a Comment