Pengine ujumbe huu ukAwa “too late” au “not applicable” kwa wazazi wako. Kubwa ni kwamba “its applicable” na “in time” kwako na kwangu. Tatizo la ajira limekua kubwa kiasi cha kutowezekana kuvumilika au kufungiwa macho tena. Binafsi kwa namna moja au nyingine naelewa sana ukubwa wa tatizo la ajira Duniani, lakini hususan kwa nchi zetu za Afrika.
Kitakwimu kama inavyoonyesha hapo chini Nchi za Afrika ni Miongoni mwa nchi zenye hali tete sana kiajira. Si kwamba mataifa yaliyoendelea hayana tatizo hili ila wao wamefaulu kwa nafasi kubwa kupambana na kupunguza tatizo hili kwa asilimia kubwa sana. Kitaalamu na watu wa Takwimu watanisahihisha nikikosea, hesabu za asilimia za viwango vya ajira hufanywa kwa kuangalia idadi ya wataalamu/wasomi waliopo ikilinganishwa na kazi zilizopo zinazolandana na field mtu aliyobobea.
Jina la Nchi
|
2011
|
2012
|
2013
|
2014
|
Ujerumani
|
5.9
|
5.4
|
5.3
|
5.0
|
India
|
3.5
|
3.6
|
3.6
|
3.6
|
China
|
3.4
|
3.3
|
3.3
|
3.2
|
Kenya
|
9.2
|
9.2
|
9.1
|
9.2
|
Nigeria
|
7.6
|
7.5
|
7.5
|
7.5
|
Spain
|
21.7
|
25.2
|
26.3
|
24.7
|
Tanzania
|
3.5
|
3.2
|
2.9
|
3.1
|
Marekani
|
9.0
|
8.2
|
7.4
|
6.2
|
Ukisafiri kwenda nje ya Afrika ni ngumu sana kuona watu wasio na ajira, na hata ukikuta mtu hana ajira kwa asilimia kubwa ni mtu kujitakia. Ila ukiangalia takwimu utakuta nchi hiyo ina asilimia kadhaa za ukosefu wa ajira. Ni kama tukichukulia mfano kupitia Tanzania; Takwimu zinaonyesha ongezeko la uchumi wa asilimia 7, ila asilimia hizo haziakisi uhalisia wa maisha. Tunajivunia awamu hii ya tano ya uongozi kwa juhudi kubwa inazofanya kuinua maisha ya mtanzania na bila shaka juhudi hizo zitafanikiwa. Mungu Mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali yake, Mjalie Ulinzi na Afya. Napongeza sana sera ya kutoa mikopo kwa wanawake na vijana katika ngazi ya kata. Ni fursa kubwa ya kujikwamua kiuchumi.
Nchi za magharibi na mashariki ya kati zimefanikiwa sana kutatua tatizo hili, kivipi wamefanikiwa?
Jambo la kwanza tuanze kwa kufahamu ukweli huu, kwamba Ongezeko la watu duniani kote linaongezeka, Vifo vya watoto wadogo ni vichache ikilinganishwa nawatoto wanaoishi, Hii ni Baraka. Kwa hiyo tutegemee Miaka 18-25 ijayo watoto wanaozaliwa leo watakua wanahitaji ajira, sijui kama hii itakua Baraka pia! Labda!... Na vilevile Vifo vya wazee havigusi sana sekta ya ajira kwani wazee wetu wengi wanaotangulia kupumnzika huwa ni baba na babu zetu au mama na bibi zetu ambao hawakua waajiriwa, hivyo hanapotangulia hawaachi fursa za kijana kuchukua nafasi hiyo.
Na utakubaliana na mimi kua wazee wetu hawa hufariki kwa kukosa matunzo au huduma muhimu kama chakula, maji safi, na dawa.
Ni wito wangu kwa vijana kama mimi ambao angalau unakuta tunao uwezo wa kutengeneza hata 3000 kwa siku au zaidi, kuangalia namna tunaweza kusaidia Bibi na Babu zetu wasioweza kujikimu kimaisha. Swala hili halihitaji serikali.
TUENDELEE NA SWALA LA AJIRA:
Nchi za Magharibi na Mashariki ya mbali zimefanya kitu naweza kukiita “family investiment”. Ni hali unakuta familia inamiliki kabiashara kadogo au hata kubwa pia. Unakuta familia inamiliki ka mgahawa, duka la samani, mashamba ya mazao, Mifugo, Halafu wanavikuza kwa kadri muda unavyoruhusu, mwisho wa siku wanaajiri mpaka watu wasio wa familia yao. Italia na Uturuki ni Moja kati ya Nchi ambazo familia zinazofanya sana uwekezaji wa migahawa.
Ukijaribu kutizama sawa utagundua kwamba ni aina ya uwekezaji ambao hata Huku kwetu Afrika unawezekana! Na kuna familia Chache zimejikwamua kiuchumi kwa namna hii, na leo hii hizi ni kati ya familia tajiri mitaani kwetu.
Pengine unaweza kuanza kujipa sababu kwamba “sisi huku Afrika baba mlevi mama ndio mpambanaji sasa hata tukiwekeza kwenye kilimo cha nyaya au makabichi, baba si atalewea zote!?” Achana na sababu za kushidwa, Hata Fid Q anasema, “Usijipe sababu za Kushindwa”… Isiwe shida tutaendelea kufundishana haya mambo kupitia Blog yetu hii “lighttz.blogspot.com”. Jinsi ya kupata misaada ya kisheria pindi mzazi mmoja wapo anaposhindwa kujukumika au jinsi social workers na watu wa community development wanavyoweza kushirikiana na familia za namna hii. Tuandikie katika ukurasa wetu wa Facebook “facebook.com/thelighttz” au tutumie email the.light.tz@gmail.com
Bila ya Familia kuhusika ni vigumu sana kutatua tatizo la ajira. Nchi za Uarabuni ni nchi za kibiashara sana na hurithishana kizazi hadi kizazi, na Hizi nchi ni moja kati ya nchi chache sana duniani zenye kiwango kidogo sana cha Ukosefu wa ajira, pengine sawa na 0.01%.
Biashara au mradi mdogo wa leo ndio kampuni au shirika kubwa la kesho litakaloajiri maelfu na mamilioni ya watu na kuchangia sana katika kuboresha huduma za kijamii na Uchumi wa taifa hata Bara kwa ujumla. Usisite kuanza kitu, hata kama hakina sura, au ni kidogo sana.
TATIZO LA AJIRA SI TATIZO LA SERIKALI, NI TATIZO LETU NA WATOTO WETU. SERIKALI YAWEZA KUONGEZA FURSA, ILA HUENDA ZISITOSHE KILA MUHITAJI. ILA FAMILIA IKIONGEZA FURSA HUWATOSHA WANAFAMILIA NA HUSOGEA HATA KUTOA NEEMA MPAKA KWA WASIO WANAFAMILIA.