Kuna umuhimu wa kufika pointi ya
kuelewa kwamba; Hakunaga miujiza kwenye swala zima la MAENDELEO na MABADILIKO.
Kama ambavyo usipokula huwezi kwenda haja, vile vile USIPOWEKEZA huwezi
KUENDELEA ama KUBADILIKA.
Mimi ni mpenzi sana wa soka,
nikiwa na washkaji zangu juzi
tukiangalia mechi kati ya German vs Czech rafiki yangu mmoja
akanifahamisha kitu ambacho kilinipa kutafakari. Kwa wale mnafuatilia soka
mtakubaliana na mimi kwamba Ujerumani inaongoza kwa ubora wa soka duniani kwa
sasa. Na ubora wao ni wa Takribani miaka 10 sasa! Na hata mpira wao ukitazama
unaona kabisa hawa watu hawajaanza leo kucheza pamoja; wanacheza kama siafu.
Je! Wafahamu ya Kuwa Asilimia 90
ya kikosi chao kiliwekewa (Naiita Software) Kichwani kwao ya kuwa na “Mission”
ya kuleta Kombe la Dunia Ujerumani tangu miaka zaidi ya 15 iliyopita? (Na
walifanikiwa mwaka 2014 kule Brazil huku mwenyeji Brazil akipigwa goli 7).
Mario Gotze, Draxler, Reus, Muller, Boateng; Wote walikuzwa chini ya “mradi” huu kwenye
academy moja. Nuer, Ozil, Podolski, Khedira nao hivyo hivyo.
Na sheria yao ujerumani ni kwamba
huwezi kuwa kocha wa Taifa kama hujawahi kufundisha timu za watoto za Ujerumani
(Academies under special projects). (kwa kuwa ndipo wanaposukia MISSION zao;
Huku kwa wakubwa ni kumalizia tu)
Sasa Pata picha tangu mtoto yuko
na miaka 5-10 na kuendelea; anachoambiwa ni kwamba kazi yako ni kuleta kombe la
dunia kwenye taifa lako! Unafkiri watakuwa wa kawaida!? Cheza yao haiwezi kuwa
ya kawaida. Kwa Nchi nyingi za Ulaya kila timu ina academy; na karibu kila
shindano kubwa lazima litanguliwe na “juniors” Under 15,17…. Tofauti sana na
huku Afrika, amabako tumeweka maslah mbele kwa kuteketeza “FUTURE” Hatuna pesa
za kuendesha UMITASHUMTA ila tunazo za kushiriki Michuano ya Kombe la Dunia!!!
Hahaha… Ni kituko sana hiki… Ni kama kumlazimisha tembo kupanda kwenye mti
Tutazame Tanzania kwa mfano;
Kipindi kile Serengeti Boys ilipoanza, kizazi cha akina Nizar Khalfan, Mrisho
Ngassa; Wakaja kuwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya Taifa! Tulijaribu
vizuri. Ni vile tu tunahitaji “A WELL DEFINED PURPOSE AND LEADERSHIP”. Nguvu
inayowekwa kwa Timu ya Taifa ya sasa, Nasikitika kusema tunamaliza pesa na
matumaini bure. Tuwaige Uganda! Walikuwaga wabovu kuliko sisi, wakatulia chini,
wakaanza kuwekeza kwa watoto, Wana wachezaji amabao wengine bado ni wanafunzi
wa vyuo vikuu na High School, kwa sasbabu ni product waliyotoka nayo tangu
udogoni. Leo hii wanamkaba koo Ghana, wanasumbua sana CECAFA na Kombe la
mataifa Afrika.
HEBU JAMANI TUJIFUNZE. HAKUNA
NJIA ZAIDI YA HII! LABDA TUNUNUE WACHEZAJI WA ACADEMY ZA ULAYA KISHA TUWAPE
URAIA.
Ni wito wetu kwa Familia, Jamii,
na Serikali; INAWEZEKANA. Ila itatuchukua muda na kweli tunahitaji muda.
Tusikimbilie kupaua ilihali hatujaweka msingi wala kufunga lenta! Academy
italeta tumaini la soka Afrika na Tanzania. Soka Lina Pesa SANA; Hebu tuamini
kuwa kipaji kinatosha. KAMA MTOTO ANA KIPAJI NA SHULE HAIWEZI, USIMPOTEZEE
MUDA. MPELEKE ACADEMY. KAMA HAKUNA ACADEMY AU HUWEZI KUGHARAMIA BASI WEKENI
UTARATIBU NA M/KITI WA KIJIJI NA DIWANI WA KUWAPA MIPIRA NA UWANJA HAWA WATOTO,
MTAANI HUKU TUNA MAKOCHA WAZURI TU. INAWEZEKANA WALA HAIHITAJI UFADHILI WA WATU
WA MAREKANI.
Wakati niko Shule ya msingi,
Nilikua nacheza mpira sana! Ila Nakumbuka watoto wenzangu ambao walikua
wakicheza unavutiwa sana kuwatazama, unaona kabisa huyu mtu ni wa kipekee!
Mnasema hakuna kama Messi na Ronaldo! Hujatembea vijijini na shule za
changanyikeni uone watoto ambao wanapiga soka kama wamezaliwa na mpira. Unaona
vitu ambavyo licha ya udogo walio nao, hata kwa Messi na Ronaldo huvioni. WAALIMU
JAMANI; MU-ORGANIZE HAWA WENYE VIPAJI HUKO MASHULENI! MWANAFUNZI ANAWEZA ASIWE
NA UWEZO DARASANI using’ang’anize ma REMIDUAL! Humsaidii… Ukifanya hivyo you
will be concentrating on her weakest point! AND WE DON’T BUILD FROM WEAKNESS;
WE BUILD FROM STRENGTH! Lazima kuna kitu yuko vizuri. HICHO HICHO KITUMIE
KUBORESHA FUTURE ALIYO NAYO! Kazi ya mwalimu sit u kumsaidie mwanafunzi afaulu
masomo ya darasani; ILA KUMSAIDIA MWANAFUNZI AJUE FUTURE ALIYONAYO NA VILE
INAVYOWEZEKANA (Naandika hapa mpaka natamani walimu wotw duniani mungeelewa
moyo wangu unachojaribu ku-communicate) Ualimu imekua kazi Fulani boring,
wengine wanasema isiyokuwa na maslah, wengine wanasema ya kudharaulika kwa
walimu wa kizazi hiki! Ila ni kwa sababu tu, hatujaweeza kuwaza nje ya chaki na
kiboko! (Naamini kwenye makala nyingine tutazungumza zaidi juu ya hili)
Nihitimishe kwa kusema;
Sisi sote ni viongozi wa swala
hili la Michezo… TUKIWEKEZA INAWEZEKANA. Mtoto asizeeke na KIPAJI chake.
0 comments:
Post a Comment