Katika historia tumejifunza vile
ambavyo kwa miaka zaidi ya 600, tulikua chini ya Ukoloni na utumwa. Willie
Lynch katika barua yake ya mwaka 1712, kuhusiana na namna alivyokusanya watumwa
alisema “Risasi tatu zinazotumika kumfanya mtu mtumwa ni: 1. HOFU, 2. KUUA
IMANI (Ile hali ya kumpotezea mtu kujiamini) na 3. WIVU.
UTUMWA ni kirusi ambacho chenyewe
hushambulia sana namna ya kufikiri ya jamii athirika. Na kisipotibiwa HUSAMBAA
NA KUENDELEA KIZAZI HADI KIZAZI; hata kama minyororo imeshafunguliwa. Hakuna ugonjwa
mbaya kama Utumwa wa fikra! Ni afadhali ule wa mijeledi na risasi.
Tazama mambo yafuatayo kisha
utaelewa dhamira yangu:
Kama umesoma shule za msingi kama
nilizosoma mimi, si jambo geni kuona mwalimu anakuja na mzigo wa fimbo
darasani. Unaweza kukumbuka hofu unayojawa nayo kama mwanafunzi? Marafiki zangu kadhaa waliacha shule! (Kwenye hili; Unadhani akili ya mwanafunzi ingeweza
kuelewa anachofundishwa?) (sasa ufikiri tu; kidogo, Je! kazi ya mwalimu ni
kuchunga ng’ombe ama kumfanya mwanafunzi awe katika ubora ambao hata mwanafunzi
mwenyewe haamini kama anaweza kuwa katika ubora huo?) Nidhamu ya saikolojia
inasema “HOFU INAUA KUJIAMINI, NA KUTOKUJIAMINI KUNAUA UWEZO” (Na hakuna
mwalimu ambaye hajasoma saikolojia, japo sio ile ya ndani sana ila ile ya kumpa
mwanga) (Ila shida iko wapi hapa!) Tuhame hapa (Waweza Kutoa maoni yako kwenye
sehemu ya “Comments”)
Wanafunzi wengi wa vyuo, haswa
wanawake wanakumbana sana na kutakwa rushwa ya ngono ili wasaidiwe kufaulu
(Mtakumbuka kile kisa cha mkufunzi aliyeshtakiwa wa chuo kimoja hivi majuzi).
Hali Fulani ya mtu kutumia nafasi aliyonayo; kwa kua anafahamu una uhitaji na
rungu kashika yeye, basi anatumia nafasi yake kukukandamiza. Tusikae sana hapa;
yako mengi ya kutazama:
Juzi askari wa kutuliza ghasia
(FFU) walitumia nguvu kubwa mno kumtia chini ya ulinzi mwanafunzi wa sekondari.
Kilikua kitendo ambacho jamii yote ya watanzania ilikilaani. Haijalishi
alifanya kosa gani ila njia iliyotumika haikua sahihi hata kidogo; hawawezi
wakakosa namna nyingine kiasi kile cha kutumia nguvu ya namna ile. Tuhame pia hapa kwa
muda
Tuje kwenye sehemu za kazi; pale
unapoenda kwenye ofisi Fulani ukihitaji huduma Fulani; vile unavyosikilizwa kwa
kuharakishwa na wakati mwingine dharau, wakati mwingine majibu yasiyo na
kufikiri; mara kwa mara toa kitu kidogo! Hii hulka na akili matope ipo kwenye
ofisi nyingi sana.
Tuje sasa kwenye kuyaconnect haya
matukio na mada yangu. Binafsi naamini “Kama kazi yako haifanyi maisha ya watu
kuwa bora; wewe ni tatizo kubwa sana kwenye huu ulimwengu! Na shida zipo kwa
sababu wewe upo”
Najua hata kama hujawahi kwenda
nchi za magharibi basi hata movie umewahi tazama! Vile askari anavyofanya kazi
yake, lugha anayotumia, mtuhumiwa anavyoelezwa na kusikilizwa! Inadhihirisha
kwamba huyu mtu anafanya hii kazi si kwa sababu alifeli darasani akakosa kazi
nyingine. Huku kwetu unaona kabisa, huyu mtu hata hii kazi ni basi tu, kuna uwezekano hii haikua kazi ya ndoto yake!
Kwa waliowahi kuvuka boda za Nchi
moja ya Afrika kwenda nchi nyingine ya afrika wanaelewa ongea na samba la afisa
na askari wa boda. Ila fika boda ya kwenda nchi za wenzetu; hadi raha yani,
hata kama kuna kitu umekosea ama hujatimiza unasaidiwa kwa moyo wote. Mpaka
unajiuliza hivi kwa nini waafrika tunachukiana hivi. Kwa nini hatupendi
mwenzetu afanikiwe? Afurahi? Tuna shida gani kwenye akili zetu?
Kwa wale mliowahi kukumbana na ofisi za usajili wa mambo kadha wa kadha; kama ardhi, kampuni, shirika n.k! Moja kati ya jambo huwa najiuliza sana ni wasajili kazi yao ni nini? Si Kusajili? Mbona kama wanavyohusika na mahitaji ya wananchi ni kama vile kazi yao si kusajili ila kuzuia usajili! Maana utawekewa kila kikwazo na kila ugumu usio wa lazima. Ni kama kuna nati imefumuka kichwani ya wao kukumbushwa kuwa kazi yao ni kinyume cha wanachofanya. kama msajili unatakiwa uhuzunike na kuumia sana na kujiona umefeli pale mwananchi anaposhindwa kusajili swala lake! Kazi ya msajili ni kuhakikisha mambo hayashindikaniki kusajiliwa. Huduma yao ni kuhakikisha wanamsaidia mwananchi kusajili swala lake (na kama hajakidhi vigezo vilivyo nje ya uwezo wake, basi asaidiwe kukidhi vigezo hivyo)
Utumwa unatuua Waafrika; Mnaonaje
wote tukaanza kufanya kazi zetu katika center ya kuhudumia watanzania na
waafrika wenzetu nao wajione kuwa watu na waone hawaishi na wajerumani ama
wakoloni wa kiingereza. Kwa nini usiipe kazi yako heshima kwa kutoa huduma kama
professional? Unadharaulika sana kwa kuwa mtumwa wa fikra.
Wewe kama mkufunzi target yako yapaswa
kuwa wanafunzi wako wawe bora kwenye ufaulu na ufanisi wa kazi.
Wewe kwa nafasi
yoyote uliyonayo yapaswa uishi kwa lengo la kazi yako kuleta amani, furaha na
utoshelevu kwa wanajamii wako!
Huko kwenu kuna watumwa? Watu
ambao wanatumia kazi zao kujiona wako juu sana kuliko wewe! Hawa ndio watumwa.
Mtu huru hutumia kazi yake kujishusha kuwa chini yako ili huduma yake ikupe
kumheshimu, Kumtambua na kumjali.
Waafrika wenzangu; kama nafasi
uliyonayo kwenye jamii ama shirika ama kampuni inakufanya kuwa COLONIAL MASTER
wewe ni muathirika wa KIRUSI CHA UJINGA Kinachoitwa UTUMWA.
Ila uzuri ni kwamba kirusi hiki KINATIBIKA! Wahi Hosipitali ya Ufahamu.
0 comments:
Post a Comment